Mmiliki wa blog hii
ndugu Ahadi A.Mwakaniemba na Mke wake Neema Ahadi wanakukaribisha
sana katika blog hii ambayo itakuwezesha kupata maarifa mbalimbali. Tutajikita
sana katika kutoa marrifa ya kilimo,ufugaji na biashara. Kupitia blog hii
kampuni ikiwa ni shamba darasa la watu kujifunza maarifa ya namna ya kufuga
kuku na nguruwe, kutengeneza bidhaa mbalimbali kama sabuni, mishumaa, Keki,
Batiki, vikoi n.k, kilimo cha mpunga, mahindi, Maharage, na bustani za
mbogamboga na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu biashara.
Kama kuna changamoto kubwa kipindi hiki
ni changamoto ya ajira. Wale ambao wana sifa za kuajiriwa hawapati nafasi ya
kuajiriwa. Pia wale ambao tayari wapo kwenye ajira, ajira zao haziwatoshelezi
kwa kipato. Kipato wanachopata kwenye ajira hizo, hakiwezi kuwawezesha kufikia
malengo yao haraka zaidi ya ajira hiyo kuwa chachu ya kuwapa nafasi ya kupanua
wigo wa vitega uchumi vingine. Na kama inavyoeleweka, changamoto ya kipato cha
ajira huchukua muda kuongezeka na hata kinapoongezeka kinaongezeka kidogo sana
hivyo akili ya kufanikiwa kwa kutegemea mshahara utajikuta unaendelea kuwa
maskini. Kwa mazingira hayo watu wasio na ajira na wale waajiriwa wanatakiwa
kuangalia njia mbadala ya kuongeza kipato chao. Kupitia biashara na shughuli mbalimbali
za ujasiriamali wanakuwa na uhakika wa kipato na kuelekea mafanikio.
Kupitia kitabu hiki utajifunza na kujua
hatua mbalimbali ili kuanzisha biashara, ukianza na namna ya kupata wazo la
biashara, uwezo mbalimbali anaotakiwa kuwa nao mjasiriamali katika kuanzisha
biashara ikiwa ni pamoja na uwezo wa kutunza kumbukumbu, uwezo wa kusimamia
fedha, uwezo wa kutafuta masoko na uwezo wa kuandika mchanganuo wa biashara ili
kurahisisha utekelezaji wa uendeshaji wa biashara, na kujua nini ufanye ili
biashara yako ikue na kuhimili ushindani unaoongezeka kila iitwapo leo katika
biashara na jinsi ambavyo utaweza kuwa mshindani kupitia njia
mbalimbali ili uweze kufikia mafanikio makubwa kupitia ujasiriamali
wako.
Mkurugenzi wa
NEA GENUINE ENTERPRISES
Ndg AHADI MWAKANIEMBA
Contacts:
Gmail: neagenuineideas@gmail.com
You tube: NEA GENUINE TV
No comments:
Post a Comment