
(Kwa nini na kwa
vipi Mungu anatuita kuongoza)
“Natufanye mtu kwa mfano wetu….. akatawale”. (Mwanzo
1:26)
Kwa karne nyingi
wakristo wamejadiliana juu ya suala la uongozi. Je, kuongoza ni kibiblia? Je,
sisi hatukuitwa ili kuwa wafuasi badala ya viongozi? Je, hatukuitwa kuwa
watumishi badala ya watawala? Je, tunaweza kuwa wakweli na kuamini kuwa uongozi
ni wazo la kibiblia?
Tunapojifunza
Biblia kwa karibu zaidi tunaona kuwa uongozi ni wazo la Mungu hasa. Si kwamba
tu Mungu ni kiongozi wa juu kabisa lakini ametuita sisi pia kuongoza.
Tumezaliwa Kuongoza
Fikiria hili. Maelezo ya mwanzo ya
mwanadamu katika Biblia yanahusisha uongozi. Mungu alituumba kuongoza, kuwa na
mamlaka na kutawala. Kulingana na Mwanzo 1:26 – 31, mimi na wewe tulizaliwa ili
kuongoza. Soma kwa undani maandiko haya …
“Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa
sura yetu, wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na
nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi”. (Mwanzo 1:26)
1.
Kuumbwa kwa mfano
wa Mungu kunamaanisha tuliumbwa ili ________.
Kulingana na
mstari wa 26, tuliumbwa kwa mfano wa Mungu. Hii inamaana gani? Kidokezo kimoja
kinapatikana katika kifungu kinachofuata “na wakatawale” Sehemu ya maana ya
kuwa mfano wa Mungu ni kujua tuliumbwa kuongoza na kutawala.
2. Mungu aliwapa wanadamu _________ juu ya
dunia yote
Tunapaswa
kujisikia vizuri juu ya nafasi mbili tulizo nazo. Nafasi ya kwanza ni kuwa
chini ya mamlaka ya Mungu. Nafasi ya pili ni kuwa na mamlaka juu ya ulimwengu.
Mungu ametupa sisi wito huu. Ni lazima tugundue ina maana gani kuongoza kama Mungu afanyavyo.
3. Kama Mungu ametuambia tutawale,
tunao________ wa kufanya hivyo.
Mungu
kamwe hatuamuru kufanya kitu bila kutupa uwezo wa kufanya kitu hicho. Wewe na
mimi tuna uwezo wa kuongoza kwa sababu Mungu alituumba na kutuamuru kufanya
hivyo. Kwa kuzingatia vipawa vyako na haiba yako una uwezo wa kuongoza katika
maeneo fulani.
Kuwa Chumvi Na Nuru
Katika
agano jipya, Mungu anathibitisha wito huu wa kuwashawishi wengine. Angalia
Mathayo 5:13-16: “Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini
hata ikolee? Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya
mlima, wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango;
nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hiyo nuru yenu na iangaze mbele ya
watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni”.
Chumvi huathiri chakula tunachokula. Nuru huathiri nyumba tunazoishi. Yesu anatuita kukumbatia wito wetu wa kushawishi na kuangaza popote tuendako. Mtume Paulo alitilia maanani wito huu pale aliposema:
“Basi tukiijua hofu ya Bwana, twawavuta wanadamu…” (2
Wakorintho 5:11)
Ruhusa ya kimungu ya kuongoza
Wengi wetu
hujisikia kama Musa alivyojisikia
alipokabiliana na Mungu katika kichaka kilichowaka moto katika Kutoka 3 – 4.
Alijisikia mpungufu na asiye na maandalizi ya kuongoza. Lakini hicho ndicho
Mungu alichomuitia kufanya. Viongozi wengi wakuu wa Biblia waliogopa na
kuukimbia wito huo. Ilibidi Mungu awape ruhusa ya kufanya hivyo.
Wengi wetu
tunaweza kutoa sababu zinazotufanya kutokuongoza vizuri, kama
Musa alivyofanya. Mungu alipomuita, mara moja, alikuwa na sababu tano za
kushindwa kuongoza. Tambua jinsi Mungu alivyojibu kuhusu sababu hizo.
Udhuru wa kwanza: Mimi ni nani? (Kutoka 3:11)
Musa alisumbuka
juu ya utambulisho wake. Hakujisikia kama alikuwa anastahili. Alifikiri Mungu
alichagua kiongozi asiye sahihi. Mwitikio wa Mungu si kitu wewe u nani.
Nimekuita. Niko pamoja na wewe.
Udhuru wa pili: Wewe ni nani? (Kutoka 3:13)
Musa alisumbuka na
uhusiano wa karibu. Hakumjua Mungu kiasi cha kutosha kumuelezea kwa watu.
Uhusiano wake na Mungu ulikuwa dhaifu. Mwitikio wa Mungu: Mimi Niko ambaye
Niko. Mimi ni kila kitu unachohitaji.
Udhuru wa tatu: Itakuwaje wasipokubali kusikiliza
(Kutoka 4:1)
Musa alisumbuka na
woga. Aliogopa juu ya mwitikio wa watu juu yake. Mwitikio wa Mungu katika
utimilifu wangu, watasikiliza. Nitumaini mimi.
Udhuru wa nne: Sijawahi kuwa mnenaji mzuri (Kutoka 4:10 )
Musa alisumbuka na
upungufu. Nani angemfuata wakati hakuweza kuzungumza vizuri? Mwitikio wa Mungu:
Fikiri nani aliufanya mdomo wako? Mimi ndiye chanzo cha vipawa vyako.
Udhuru wa tano: Najua unaweza kupata mwingine (Kutoka 4:13 )
Musa alisumbuka na
kujidharau. Alijilinganisha na watu wengine wenye uwezo zaidi yake na akajiona
hafai. Mwitikio wa Mungu. Sawa, utakwenda na Haruni… lakini bado nakuita wewe.
SWALI: Una udhuru
gani kwa kutokuongoza vizuri? Unaamini mwitikio wa Mungu waweza kuwaje?
Amka sasa
No comments:
Post a Comment