Wito Wa Mungu
Kwetu Wa Kuongoza
“Natufanye mtu kwa mfano wetu…..
akatawale”. (Mwanzo 1:26)
Kwa karne nyingi wakristo wamejadiliana
juu ya suala la uongozi. Je, kuongoza ni kibiblia? Je, sisi hatukuitwa ili kuwa
wafuasi badala ya viongozi? Je, hatukuitwa kuwa watumishi badala ya watawala?
Je, tunaweza kuwa wakweli na kuamini kuwa uongozi ni wazo la kibiblia?
Tunapojifunza Biblia kwa karibu zaidi
tunaona kuwa uongozi ni wazo la Mungu hasa. Si kwamba tu Mungu ni kiongozi wa
juu kabisa lakini ametuita sisi pia kuongoza.
Tumezaliwa Kuongoza
Fikiria
hili. Maelezo ya mwanzo ya mwanadamu katika Biblia yanahusisha uongozi. Mungu
alituumba kuongoza, kuwa na mamlaka na kutawala. Kulingana na Mwanzo 1:26 – 31,
mimi na wewe tulizaliwa ili kuongoza. Soma kwa undani maandiko haya …
“Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano
wetu, kwa sura yetu, wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na
wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi”.
(Mwanzo 1:26)
1. Kuumbwa kwa mfano wa Mungu kunamaanisha tuliumbwa ili ________.
Kulingana na mstari wa 26, tuliumbwa kwa
mfano wa Mungu. Hii inamaana gani? Kidokezo kimoja kinapatikana katika kifungu
kinachofuata “na wakatawale” Sehemu ya maana ya kuwa mfano wa Mungu ni kujua
tuliumbwa kuongoza na kutawala.
2. Mungu
aliwapa wanadamu _________ juu ya dunia yote
Tunapaswa
kujisikia vizuri juu ya nafasi mbili tulizo nazo. Nafasi ya kwanza ni kuwa
chini ya mamlaka ya Mungu. Nafasi ya pili ni kuwa na mamlaka juu ya ulimwengu.
Mungu ametupa sisi wito huu. Ni lazima tugundue ina maana gani kuongoza kama Mungu
afanyavyo.
3. Kama Mungu ametuambia tutawale, tunao________ wa kufanya hivyo.
3. Kama Mungu ametuambia tutawale, tunao________ wa kufanya hivyo.
Mungu
kamwe hatuamuru kufanya kitu bila kutupa uwezo wa kufanya kitu hicho. Wewe na
mimi tuna uwezo wa kuongoza kwa sababu Mungu alituumba na kutuamuru kufanya
hivyo. Kwa kuzingatia vipawa vyako na haiba yako una uwezo wa kuongoza katika
maeneo fulani.
Kuwa Chumvi Na
Nuru
Katika agano jipya, Mungu anathibitisha wito huu wa kuwashawishi wengine.
Angalia Mathayo 5:13-16: “Ninyi ni
chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee?
Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima, wala
watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo
yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hiyo nuru yenu na iangaze mbele ya
watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni”.
Chumvi huathiri chakula tunachokula. Nuru huathiri nyumba tunazoishi. Yesu anatuita kukumbatia wito wetu wa kushawishi na kuangaza popote tuendako. Mtume Paulo alitilia maanani wito huu pale aliposema:
“Basi tukiijua hofu ya Bwana, twawavuta
wanadamu…” (2
Wakorintho 5:11)
Ruhusa ya kimungu ya kuongoza
Wengi wetu hujisikia kama Musa
alivyojisikia alipokabiliana na Mungu katika kichaka kilichowaka moto katika
Kutoka 3 – 4. Alijisikia mpungufu na asiye na maandalizi ya kuongoza. Lakini
hicho ndicho Mungu alichomuitia kufanya. Viongozi wengi wakuu wa Biblia
waliogopa na kuukimbia wito huo. Ilibidi Mungu awape ruhusa ya kufanya hivyo.
Wengi wetu tunaweza kutoa sababu
zinazotufanya kutokuongoza vizuri, kama Musa
alivyofanya. Mungu alipomuita, mara moja, alikuwa na sababu tano za kushindwa
kuongoza. Tambua jinsi Mungu alivyojibu kuhusu sababu hizo.
Udhuru wa kwanza: Mimi ni nani? (Kutoka
3:11)
Musa alisumbuka juu ya utambulisho wake.
Hakujisikia kama alikuwa anastahili. Alifikiri Mungu alichagua kiongozi asiye
sahihi. Mwitikio wa Mungu si kitu wewe u nani. Nimekuita. Niko pamoja na wewe.
Udhuru wa pili: Wewe ni nani? (Kutoka 3:13)
Musa alisumbuka na uhusiano wa karibu.
Hakumjua Mungu kiasi cha kutosha kumuelezea kwa watu. Uhusiano wake na Mungu
ulikuwa dhaifu. Mwitikio wa Mungu: Mimi Niko ambaye Niko. Mimi ni kila kitu
unachohitaji.
Udhuru wa tatu: Itakuwaje wasipokubali
kusikiliza (Kutoka 4:1)
Musa alisumbuka na woga. Aliogopa juu ya
mwitikio wa watu juu yake. Mwitikio wa Mungu katika utimilifu wangu,
watasikiliza. Nitumaini mimi.
Udhuru wa nne: Sijawahi kuwa mnenaji mzuri
(Kutoka 4:10 )
Musa alisumbuka na upungufu. Nani
angemfuata wakati hakuweza kuzungumza vizuri? Mwitikio wa Mungu: Fikiri nani
aliufanya mdomo wako? Mimi ndiye chanzo cha vipawa vyako.
Udhuru wa tano: Najua unaweza kupata
mwingine (Kutoka 4:13 )
Musa alisumbuka na kujidharau.
Alijilinganisha na watu wengine wenye uwezo zaidi yake na akajiona hafai.
Mwitikio wa Mungu. Sawa, utakwenda na Haruni… lakini bado nakuita wewe.
SWALI: Una udhuru gani kwa kutokuongoza
vizuri? Unaamini mwitikio wa Mungu waweza kuwaje?
IJUE NAFASI AMBAYO MUNGU AMEKUPA
No comments:
Post a Comment