Monday, July 23, 2018

MAFANIKIO NA VYANZO VYAKE

MISINGI YA KUFIKIA MAFANIKIO YA KIUCHUMI
Ninakusalimu tena kwa jina la Yesu ! 
 Katika maisha ya mwilini wakristo tunatakiwa kuwa namafanikio
 mazuri ili tuweze kutimiza kusudi la Mungu. Mfano
Isaya 58:7-12, Mathayo 25:35-36 .
Huu ndio msingi wa mafanikio haya:

 a.   Akili/fikra
Fikra ni mkusanyiko na mtiririko wa mawazo unaotengeneza msimamo wa kiutekelezaji ndani ya mtu. Fikra inaonyesha ulivyo kimaisha. Inaonyesha kiwango chako cha kufikiri kilipo au kilipofika.

Ni ukweli kwamba kila binadamu ana akili ya kung'amua jema na baya ila sio wote wanaojua thamani ya akili walizonazo. Wapo wanaozitumia kwa faida na malengo na kupata mafanikio pia wapo wanaozitumia vibaya na kuishia kuishi maisha ya shida hadi wanakufa kwa umaskini. Tuzitumie akili zetu katika kujituma na kufikiri kwa utofauti na wanavyofiki wengine. Tuwe tayari kujifunza kwa wenye elimu juu ya kile tunataka kufanya na sio kuiga wanavyofanya watu wengine.

1Wakorintho 15:34

Katika kuitumia akili ndipo huonekana tofauti ya wanaojua na wasiojua kitu. Ili ufanikiwe lazima akili zako utumie kufikiri na kuamua ni nini ufanye, namna gani na wakati gani. Ili kuonyesha matumizi sahihi ya akili kila binadamu anatakiwa kufikiri na kuwaza kabla ya kuamua kufanya jambo lolote katika maisha yake.

b. Muda.

Kila binadamu ana muda na amepewa muda wa kuishi na kufanya mambo yake kwa uhuru na amani. Lakini si watu wote wanaoutumia muda wao vizuri katika kujipatia mafanikio.

Muda ndio rasilimali muhimu kuliko zote ukiutumia vizuri hakika utafanikiwa. Jiulize kuna tofauti gani kati ya tajiri na masikini katika muda? Kila mtu ana masaa 24 tofauti ni matumizi tu

Ukafatilia utagundua, tajiri ana panga malengo na mipangilio yake katika siku wakati maskini hana mipangilio. Jiangalie vizuri unatumiaje muda wako ili kuyafikia mafanikio yako unayotamani uwe nayo. Kuna uhusiano mkubwa kati ya muda na uthamani katika kufikia malengo yako na usipoangalia utajikuta mafanikio yako hayaji kwa wakati.

c. Kipawa / kipaji.

Huu ni uwezo wa ndani alionao kila binadamu bila kujali kabila lake au rangi yake ana kile anachoweza kukifanya tofauti na wenzake. Hicho ndicho kipaji na mtu akikigundua na kukitumia vizuri hupata mafanikio.

Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; Kila kigeukapo hufanikiwa. Mithali 17:8

Siku zote tafuta kujua kipaji chako na kitumie upate utajiri na mafanikio katika maisha yako. Unapokuwa na kipaji na ukikitumia ipasavyo mafanikio makubwa yanakuwa upande wako.

d. Nguvu.

Kila mtu amepewa nguvu na uwezo wa kufanya jambo fulani. Tunaweza kuzitumia nguvu zetu katika kilimo, biashara na hata kazi yeyote halali na kujipatie kitu tunachataka katika maisha. Si rahisi tulale tuamke kesho matajiri bila kufanya kazi.

Vijana wengi utakuta wanataka kufanya kazi rahisi na kupata faida kubwa. Mafanikio ni mchakato, ni safari. Hivyo ili upate utajiri kubali kutumia nguvu zako.

e. Watu.

Kila mtu iwe kwa kutaka au kutotaka amezungukwa na jamii ya watu. Na kimsingi umepewa watu hao na Mungu ili uweze kuwatumia na kupata kile unachotaka/kuhitaji katika maisha yako.

Lakini kutokana na watu hawa unaweza na unapaswa uwatumie katika ushauri na maarifa waliyonayo ili kupata kile unachotaka ambacho si kingine ni mafanikio. Kushindwa kwako kuwatumia watu hawa hili litakuwa ni tatizo lingine ambapo ukishindwa kufanikiwa usimlaumu mtu.

Kwa kuwa na vitu hivyo unakuwa na msingi mkubwa wa kufanikiwa, na hivyo katika kufanikiwa uvumilivu ni sifa moja wapo ya mtu anayetaka kufanikiwa. Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.  Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli? (Luka 16:10-11)


Pamoja na kuwa na vitu hivi vya msingi bila mambo haya bado utabaki kama ulivyo.
1.Kuwa na maono.  
Maono ni picha ya maisha yako ya baadaye au 

Ni picha kubwa ya namna unavyoona baadaye yako.

The big picture of the preferable future.

 Mwanzo 29:15-20, Mwanzo 21:14-19, Waefeso 1:15-19 

Usipoona picha ya baadaye au usipopanga namna 

uunavyotaka baadaye yako iwe unachokifanya ndicho 

kitakachoamua baadaye yako. Mungu hakupi kitu

 usichokiona. AngaliaMwanzo 13:14   
2.  Kuwa na malengo 
  • Malengo, Husababisha msaada wa Mungu kutokea Ayubu 22:28 
  • Malengo hukupa nidhamu ya kimaisha Mwanzo 29:16-18, Mithali 29:18 
3.   Kuwa na mipango
Mipango na Bajeti Upangaji mipango ni mchakato unaoweka malengo, kubainisha rasilimali zilizopo/uwezo na mikakati itakayotumika kufikia malengo katika kipindi maalumu. Mara uandaaji wa mpango unapokamilika kinachofuata ni utekelezaji.  Katika utekelezaji baadhi ya malengo yaliyowekwa katika mpango yanafikiwa na mengine hayafikiwi katika muda uliokusudiwa. Pia kadiri wakati unavyoenda ndiyo vipaumbele vipya vinavyoibuka kutokana na mabadiliko katika nyanja mbalimbali kijamii na kiuchumi.  Hivyo basi, ipo haja ya kufanya mapitio mara kwa mara ili kuihuisha mipango, kwa kubaini utekelezaji ulipofikia na kuingiza vipaumbele vipya.  Kwa msingi huu, mapitio ni sehemu muhimu katika mchakato wa upangaji mipango. 

Madhumuni ya kupanga

 • Kuwezesha utekelezaji wa shughuli katika utaratibu unaokubalika ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

• Kuweza kufahamu rasilimali zilizopo ili kukabiliana na Vikwazo.

 • Kuweza kubinisha mahitaji ya Jamii. 

Faida za kupanga 

• Kupanga kunawezesha mgawanyo muafaka wa rasilimali chache zilizopo

 • Kupanga kunawezesha utekelezaji wa shughuli kwa wakati.

• Mpango ni zana inayoongoza katika usimamizi wa shughuli za maendeleo.  



Umebarikiwa kwa kuwa una maono.Tembea katika hayo ufanikiwe.

No comments:

Post a Comment

MAENDELEO

           JINSI YA KUANZISHA BIASHARA Uchumi wa Tanzania umekuwa ukizalisha ajira chache kila siku. Hii imekuwa ikifanya vijana wengi wa...