Monday, March 11, 2019

           JINSI YA KUANZISHA BIASHARA
Uchumi wa Tanzania umekuwa ukizalisha ajira chache kila siku. Hii imekuwa ikifanya vijana wengi wanaohitimu vyuoni kubaki wakizunguka na bahasha kila kona kusaka ajira.
Takwimu kutoka ofisi ya takwimu ya taifa zinaonyesha kuwa mwaka 2014 taifa lilizalisha nafasi za ajira 282,382 tu ukilinganisha na mahitaji ya zaidi ya wahitimu 400,000 wanaomaliza vyuo kila mwaka.
Hii inaonyesha dhahiri kuwa Tanzania kama nchi inahitaji kuweka nguvu za ziada katika kuhakikisha kuwa nafasi zaidi za ajira zinatengenezwa.
Pengine njia pekee inayoweza kutumiwa kupunguza tatizo hili au hata kulimaliza kabisa ni kupitia ajira binafsi (Ujasiriamali).
Pamoja na kuwa ujasiriamali unaweza kuwa suluhisho la ajira nchini, vijana wengi wameshindwa kabisa kufanya ujasiriamali kutokana na kukosa elimu sahihi. Kwa bahati mbaya sana mfumo wetu wa elimu haumsaidii sana muhitimu kupata stadi za ujasiriamali.
Katika vipaumbele vyake, Rais John Magufuli anasisitiza sana Tanzania ya viwanda, lakini hili litatokea tu kama vijana wa kitanzania watapatiwa elimu ya ujasiriamali.
Sehemu hii itakuwa ikiwapatia makala mbalimbali za ujasiriamali… tutajifunza jinsi ya kuanzisha biashara, jinsi ya kuendeleza biashara yako na namna ya kupata fedha.
Leo tutaanza kujifunza mambo ya msingi katika kuanzisha biashara.
Mambo ya Msingi katika kuanzisha biashara
Biashara yoyote huanza na wazo, ila wazo pekee halitoshi, linahitaji kufanyiwa kazi. Hapo ndipo watu wengi huweza kuanza kujisikia kuzidiwa. Si ajabu kuona mtu anakatishwa tamaa kwa kutizama msururu wa mambo yanayohitajika ili kuanzisha biashara, lakini pia kuanzisha biashara ni rahisi kuliko unavyodhani. Kama ilivyo katika lengo lolote kubwa, ukianza kwa kutengeneza malengo madogo madogo ya kutekeleza utaweza kufanya mambo yote muhimu katika kuanzisha biashara.

Jinsi ya Kuanzisha Biashara Ndogo
Kuanzisha na kuendesha biashara inahitaji msukumo, nia na kipaji. Inahitaji pia utafiti na mipango. Kama ilivyo kwenye mchezo wa drafti, mafanikio kwenye biashara ndogo huanza na maamuzi sahihi katika hatua za mwanzoni. Ikumbukwe pia hapa kuwa pamoja na kwamba makosa madogomadogo ya mwanzoni yanaweza yasiue biashara yako, inahitaji ujuzi, nidhamu, na bidii kuyasahihisha.
Ili kuboresha uwezekano wa kufanikiwa, unapaswa kutenga muda wa kujichunguza na kutathmini malengo yako kibiashara na malengo binafsi. Tumia taarifa hiyo kutengeneza kwa umakini mkubwa mpango wa biashara ambao utakuwezesha kufikia malengo yako.
Mchakato wa kuandaa mchanganuo wa biashara utakuchochea kufikiria hata baadhi ya mambo ambayo usingekumbuka kuyafikiria katika hali ya kawaida. Mchanganuo wako utakuwa zana muhimu sana unapopambana kutafuta fedha kwa ajili ya biashara yako. Mchanganuo huo pia unaweza kutumika kama kigezo cha kila mara kufuatilia/ kupima mafanikio ya biashara yako.
Yako mambo kadhaa yanayohitajika katika biashara yoyote.
Jambo la kwanza kabla ya kuanzisha biashara ni kuwa unatakiwa ujiulize sababu za wewe kutaka kuingia kwenye biashara. Sababu zilizozoeleka za kuanza biashara ni:
  • Unataka kujiongoza mwenyewe.
  • Unataka uhuru wa kifedha.
  • Unataka uhuru wa kutumia ubunifu wako.
  • Unataka kutumia kikamilifu ujuzi na ufahamu wako
Jambo la pili ni kuamua biashara ipi inakufaa? Ili kufahamu ni biashara ipi inakufaa, jiulize maswali yafuatayo:
  • Ninapenda kutumiaje muda wangu?
  • Nimejifunza au kusomea ujuzi gani?
  • Watu wengine wanazungumzia ubora wangu kwenye mambo gani?
  • Nina muda kiasi gani kuendesha biashara kwa ufanisi?
  • Katika mambo ninayopendelea yapo ambayo yanaweza yakawa fursa ya biashara?
  • Biashara yangu itahudumia sehemu/ kundi gani katika soko?
  • Je? Wazo langu linatekelezeka na litakidhi hitaji katika soko?
  • Ushindani nilionao ni upi? Nami nina uwezo gani katika ushindani?
  • Biashara yangu ina manufaa gani kuzidi zingine zilizopo?
  • Je? Naweza kutoa huduma zenye ubora zaidi?
  • Je? Naweza kutafuta soko kwa ajili ya bidhaa/ huduma zangu?
Ukishapata majibu ya maswali hayo hapo juu ni wazi kuwa utakuwa ulishaanza kujua ni biashara gani unaweza kuianzisha. Lakini pia unatakiwa ujiulize maswali haya hapa ili kuwa na uhakika na biashara ambayo utaifanya.
  • Ninakusudia kuanzisha Biashara gani?
  • Nitauza bidhaa gani au nitatoa huduma gani? Biashara nitafanyia eneo gani?
  • Nitatumia ujuzi na uzoefu gani kwenye biashara?
  • Biashara yangu itakuwa na muundo gani kisheria?
  • Niiite biashara yangu jina gani?
  • Nitatumua vifaa gani, na nitakuwa na mahitaji gani?
  • Nahitaji bima ya aina gani?
  • Nahitaji fedha kiasi gani?
  • Nina rasilimali zipi?
  • Nitajilipaje?
Majibu yako yatasaidia kutengeneza mpango makini, uliofanyiwa utafiti wa kutosha, ambao utautumia kama ramani ya kuelekeza kila hatua katika utekelezaji wa biashara na hata kupata mtaji.

Chagua muundo sahihi wa biashara yako.
Unapoanzisha biashara yoyote, mojawapo ya maamuzi muhimu sana ya kufanya ni uchaguzi wa muundo wa hiyo biashara. Mambo yanayozingatiwa katika kuchagua muundo wa biashara ni pamoja na:
  • Masharti ya kisheria
  • Uwajibikaji wa wamiliki kwa madeni ya biashara
  • Aina ya shughuli za biashara
  • Mgawanyo wa mapato
  • Mahitaji ya mtaji
  • Idadi ya wafanyakazi na utawala
  • Manufaa na hasara za kihasibu/ kikodi
  • Urefu wa mzunguko wa biashara

Monday, July 23, 2018

VITA VIZURI

Vita Vizuri

Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda. Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake. 2 Timotheo 4:7,8


K
atika kipindi kirefu cha utumishi, kamwe Paulo hakusita katika utii wake kwa Mwokozi. Popote alipokuwa—iwe ni mbele za Mafarisayo wenye hasira, au mamlaka ya Kirumi; mbele za kundi lenye hasira pale Listra au wenye dhambi walioamini kwenye gereza la shimoni la Makedonia; iwe ni kutoa hoja kwa mabaharia walioshikwa na hofu kwenye mashua iliyovunjika, au kusimama peke yake mbele za Nero kutetea maisha yake—kamwe alikuwa hajawahi kujisikia kuaibika kutetea kile alichokiamini. Kusudi moja kuu la maisha yake ya Kikristo lilikuwa kumtumikia Yeye ambaye jina lake lilimjaza kwa dharau; na kutokana na kusudi hili, hakuna upinzani au mateso ambayo yaliweza kumgeuzia upande mwingine.

Maisha ya Paulo ni mfano wa ukweli aliokuwa akiufundisha na hapa ndipo tunapoona nguvu yake. Moyo wake ulikuwa umejawa na hisia yenye kina ya wajibu wake naye alifanya kazi kwa mawasiliano ya karibu zaidi na Mungu aliye chemchemi ya haki, rehema na kweli….Upendo wa Mwokozi ulikuwa ndiyo dhamira isiyokufa ambayo ilimshikilia kwenye mapambano yake dhidi ya nafsi na kwenye vita vyake dhidi ya uovu kama alivyokuwa kwenye utumishi wa Kristo akisonga mbele dhidi ya kutokuwa rafiki wa dunia na upinzani wa maadui zake.

Kile kanisa linachohitaji katika siku hizi za hatari ni jeshi la watendakazi ambao, kama Paulo, wamejifunza ili wawe wenye manufaa, ambao wana uzoefu wa kina katika mambo ya Mungu na ambao wamejawa na bidii na ari. Watu waliotakaswa, wanaojitoa wanahitajika; watu ambao hawatajitenga na majaribio na wajibu; watu walio jasiri na wakweli; watu ambao mioyoni mwao Kristo ameumbika “tumaini la utukufu,” naye ambaye midomo yake imeguswa kwa moto mtakatifu ata“lihubiri neno.”…

Je, vijana wetu watakubali hii amana takatifu itokayo mikononi mwa baba zetu? Wanajiandaa kujaza nafasi inayoachwa kutokana na kifo cha aliye mwaminifu? Maagizo ya mtume yatatiliwa maanani, mwito kwa ajili ya wajibu utasikiwa, katikati ya uchochezi wa ubinafsi na tamaa zinazowavutia vijana?

MAFANIKIO NA VYANZO VYAKE

MISINGI YA KUFIKIA MAFANIKIO YA KIUCHUMI
Ninakusalimu tena kwa jina la Yesu ! 
 Katika maisha ya mwilini wakristo tunatakiwa kuwa namafanikio
 mazuri ili tuweze kutimiza kusudi la Mungu. Mfano
Isaya 58:7-12, Mathayo 25:35-36 .
Huu ndio msingi wa mafanikio haya:

 a.   Akili/fikra
Fikra ni mkusanyiko na mtiririko wa mawazo unaotengeneza msimamo wa kiutekelezaji ndani ya mtu. Fikra inaonyesha ulivyo kimaisha. Inaonyesha kiwango chako cha kufikiri kilipo au kilipofika.

Ni ukweli kwamba kila binadamu ana akili ya kung'amua jema na baya ila sio wote wanaojua thamani ya akili walizonazo. Wapo wanaozitumia kwa faida na malengo na kupata mafanikio pia wapo wanaozitumia vibaya na kuishia kuishi maisha ya shida hadi wanakufa kwa umaskini. Tuzitumie akili zetu katika kujituma na kufikiri kwa utofauti na wanavyofiki wengine. Tuwe tayari kujifunza kwa wenye elimu juu ya kile tunataka kufanya na sio kuiga wanavyofanya watu wengine.

1Wakorintho 15:34

Katika kuitumia akili ndipo huonekana tofauti ya wanaojua na wasiojua kitu. Ili ufanikiwe lazima akili zako utumie kufikiri na kuamua ni nini ufanye, namna gani na wakati gani. Ili kuonyesha matumizi sahihi ya akili kila binadamu anatakiwa kufikiri na kuwaza kabla ya kuamua kufanya jambo lolote katika maisha yake.

b. Muda.

Kila binadamu ana muda na amepewa muda wa kuishi na kufanya mambo yake kwa uhuru na amani. Lakini si watu wote wanaoutumia muda wao vizuri katika kujipatia mafanikio.

Muda ndio rasilimali muhimu kuliko zote ukiutumia vizuri hakika utafanikiwa. Jiulize kuna tofauti gani kati ya tajiri na masikini katika muda? Kila mtu ana masaa 24 tofauti ni matumizi tu

Ukafatilia utagundua, tajiri ana panga malengo na mipangilio yake katika siku wakati maskini hana mipangilio. Jiangalie vizuri unatumiaje muda wako ili kuyafikia mafanikio yako unayotamani uwe nayo. Kuna uhusiano mkubwa kati ya muda na uthamani katika kufikia malengo yako na usipoangalia utajikuta mafanikio yako hayaji kwa wakati.

c. Kipawa / kipaji.

Huu ni uwezo wa ndani alionao kila binadamu bila kujali kabila lake au rangi yake ana kile anachoweza kukifanya tofauti na wenzake. Hicho ndicho kipaji na mtu akikigundua na kukitumia vizuri hupata mafanikio.

Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; Kila kigeukapo hufanikiwa. Mithali 17:8

Siku zote tafuta kujua kipaji chako na kitumie upate utajiri na mafanikio katika maisha yako. Unapokuwa na kipaji na ukikitumia ipasavyo mafanikio makubwa yanakuwa upande wako.

d. Nguvu.

Kila mtu amepewa nguvu na uwezo wa kufanya jambo fulani. Tunaweza kuzitumia nguvu zetu katika kilimo, biashara na hata kazi yeyote halali na kujipatie kitu tunachataka katika maisha. Si rahisi tulale tuamke kesho matajiri bila kufanya kazi.

Vijana wengi utakuta wanataka kufanya kazi rahisi na kupata faida kubwa. Mafanikio ni mchakato, ni safari. Hivyo ili upate utajiri kubali kutumia nguvu zako.

e. Watu.

Kila mtu iwe kwa kutaka au kutotaka amezungukwa na jamii ya watu. Na kimsingi umepewa watu hao na Mungu ili uweze kuwatumia na kupata kile unachotaka/kuhitaji katika maisha yako.

Lakini kutokana na watu hawa unaweza na unapaswa uwatumie katika ushauri na maarifa waliyonayo ili kupata kile unachotaka ambacho si kingine ni mafanikio. Kushindwa kwako kuwatumia watu hawa hili litakuwa ni tatizo lingine ambapo ukishindwa kufanikiwa usimlaumu mtu.

Kwa kuwa na vitu hivyo unakuwa na msingi mkubwa wa kufanikiwa, na hivyo katika kufanikiwa uvumilivu ni sifa moja wapo ya mtu anayetaka kufanikiwa. Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.  Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli? (Luka 16:10-11)


Pamoja na kuwa na vitu hivi vya msingi bila mambo haya bado utabaki kama ulivyo.
1.Kuwa na maono.  
Maono ni picha ya maisha yako ya baadaye au 

Ni picha kubwa ya namna unavyoona baadaye yako.

The big picture of the preferable future.

 Mwanzo 29:15-20, Mwanzo 21:14-19, Waefeso 1:15-19 

Usipoona picha ya baadaye au usipopanga namna 

uunavyotaka baadaye yako iwe unachokifanya ndicho 

kitakachoamua baadaye yako. Mungu hakupi kitu

 usichokiona. AngaliaMwanzo 13:14   
2.  Kuwa na malengo 
  • Malengo, Husababisha msaada wa Mungu kutokea Ayubu 22:28 
  • Malengo hukupa nidhamu ya kimaisha Mwanzo 29:16-18, Mithali 29:18 
3.   Kuwa na mipango
Mipango na Bajeti Upangaji mipango ni mchakato unaoweka malengo, kubainisha rasilimali zilizopo/uwezo na mikakati itakayotumika kufikia malengo katika kipindi maalumu. Mara uandaaji wa mpango unapokamilika kinachofuata ni utekelezaji.  Katika utekelezaji baadhi ya malengo yaliyowekwa katika mpango yanafikiwa na mengine hayafikiwi katika muda uliokusudiwa. Pia kadiri wakati unavyoenda ndiyo vipaumbele vipya vinavyoibuka kutokana na mabadiliko katika nyanja mbalimbali kijamii na kiuchumi.  Hivyo basi, ipo haja ya kufanya mapitio mara kwa mara ili kuihuisha mipango, kwa kubaini utekelezaji ulipofikia na kuingiza vipaumbele vipya.  Kwa msingi huu, mapitio ni sehemu muhimu katika mchakato wa upangaji mipango. 

Madhumuni ya kupanga

 • Kuwezesha utekelezaji wa shughuli katika utaratibu unaokubalika ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

• Kuweza kufahamu rasilimali zilizopo ili kukabiliana na Vikwazo.

 • Kuweza kubinisha mahitaji ya Jamii. 

Faida za kupanga 

• Kupanga kunawezesha mgawanyo muafaka wa rasilimali chache zilizopo

 • Kupanga kunawezesha utekelezaji wa shughuli kwa wakati.

• Mpango ni zana inayoongoza katika usimamizi wa shughuli za maendeleo.  



Umebarikiwa kwa kuwa una maono.Tembea katika hayo ufanikiwe.

NGUVU ILIYO KWENYE ULIMI

GUVU YA ULIMI (MANENO) KATIKA KUAMUA HATMA YA MAISHA YAKO



Mada: Mambo muhimu kujua kuhusu matumizi ya kinywa
Katika sehemu ya kwanza nilikuonyesha mistari mbalimbali kutoka kwenye Biblia inavyozungumza kwa habari ya ulimi ili upate kujua nguvu ya ulimi ilivyo na athari zake. Ili kusoma sehemu ya kwanza tafadhali bonyeza link ifuatayo https://sanga.wordpress.com/2017/01/31/nguvu-ya-maneno-katika-kuamua-hatma-ya-maisha-yako-sehemu-ya-kwanza/
Katika sehemu hii ya pili na ya mwisho nitafundisha mambo muhimu kuzingatia na kujua kwa habari ya matumizi ya ulimi (kinywa) ili kuweka hatma nzuri ya maisha yako kwa sababu maneno yako yana nguvu ya kuathiri maisha yako ya sasa na baadaye pia.
  • Jifunze kuzuia ulimi wako usinene mabaya – Mtume Petro anatueleza kwamba Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila’ (1Petro 3:10). Ikiwa unataka kuwa na maisha yenye furaha na amani (siku njema) basi chunga sana unayoyasema. Ukiruhusu kinywa chako kunena mabaya na kutunga hila usitegemee kuwa na amani ya kweli, maana utaishi kwa maneno hayo. Daima usiakiache kinywa chako kinene mabaya wala kutunga hila kwa kuwa mtu azuiaye kinywa chake kunena mabaya, huilinda nafsi yake na taabu (Rejea Mithali 21:23 & Zaburi 50:19). Kumbuka unaponena mabaya juu ya mwingine, kama mtu huyo hana Yesu aliye hai wa kumuongoza kusamehe, basi ujue ndani yake unaamsha roho ya kisasi na uharibifu. Wapo pepo ambao kazi yao ni kufuatilia nini mtu anajinenea au kunena juu ya mwingine hususani yale ambayo ni mabaya, na kazi yao kufuatilia maneno hayo kuhakikisha kwamba yanatimia au yanatokea.
  • Jizuie kunena unapokuwa na hasira – Katika Waefeso 4: 26 imeandikwa Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka’. Mara nyingi kwenye jambo hili watu wengi wameshindwa kujizuia, na ukitaka ujue yaujazayo moyo wa mtu au mtu anakuwazia nini subiri azungumze habari zako au mambo yako akiwa amekasirika.  Hasira ni mlango ambao adui anautumia sana kuharibu maisha ya watu wengi na hasa wanandoa kwa sababu ya yale ambayo kila mmoja aliyanena akiwa na hasira na uchungu juu ya mwenzake. Biblia inatuambia kunyamaza ni hekima, hivyo jifunze kunyamaza. Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu’ (Mithali 17:28).

  • Jifunze kulinda kinywa chako – ukienda kwenye Mithali 13:3 Biblia inasema ‘Yeye alindaye kinywa chake hulinda nafsi yake, bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu’. Naam watu wengi hawajui kwamba kadri unavyosema maneno mabaya, ya uongo, kusengenya au kusingiza au kuchafua nk, ndivyo wanavyojitengenezea mazingira ya uharibifu kwenye maisha yao binafsi na si tu kwa wale ambao wanawaelekezea maneno husika.Katika Mithali 21:23 imeandikwa ‘Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, Atajilinda nafsi yake na taabu’Hii ni kwa sababu maneno unayoyanena unayaumba au kuyaandika na kwa jinsi hiyo maneno hayo yana nguvu ya kuongoza na kuathiri hisia, nia na maamuzi (matendo) yako.
  • Jifunze kuwa mtu wa maneno machache – Biblia inatuambia ‘Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili’ (Mithali 10:19). Naam sio lazima kusema kila neno linalokujia jifunze kunyamaza na kuzuia maneno yako, maana azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa. Ingawa Yakobo anatuambia ulimi haufugiki, lakini kwa mujibu wa (Mithali 17:27a) mtu anaweza kuzuia maneno yake na hiki ndicho alichomaanisha Mzee Yakobo mwenyewe pale aliposema iweni wepesi wa kusikia na si wepesi wa kusema (Yakobo 1:19).
  • Jifunze kufikiri kabla hujanena – Katika Mithali 12:18 imeandikwa ‘Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya. Naamini umeshawahi kupitia mazingira ambayo unajutia maneno uliyoyanena. Mara nyingi majuto hayo ni matokeo ya kunena bila kufikiri. Hii ina maana kabla ya kusema, jifunze kufikiri kwanza athari ya unachotaka kusema kwa mtu au watu unaotaka kusema nao. Katika kufanikisha hili mwimbaji wa Zaburi akasema Ee Bwana, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu’ (Zaburi 141:3).
  • Jaza neno la Mungu moyoni mwako (Yoshua 1:8) – Hii ni kwa sababu yale yaujazayo moyo wa mtu ndiyo yamtokayo. Hivyo ili kusaidia kinywa chako kutoa maneno yenye kujenga sharti neno la Mungu likae kwa wingi moyoni. Hatutegemei mtu aliyejaa neno la Mungu atukane watu, kulaani, kusengenya nk. Katika Yakobo 3:9-10 imeandikwa ‘Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu. Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo’. Naam ile kusema haifai mambo hayo kuwa hivyo ni ishara kwamba hatupaswi kutumia vinywa vyetu kunena mabaya na kutunga hila wakati tunatumia pia ulimi huo huo kumtukuza Mungu.
Katika kumalizia ujumbe huu sina budi kusema mwanadamu hana budi kuwa makini sana na kinywa chake. Maisha ya mtu yanachangiwa kwa sehemu kubwa na maneno yake, akiutumia vizuri ulimi wake  ataishi vizuri na akiutumia vibaya mabaya yatakuwa haki yake. Naamini ujumbe huu mfupi umekuongezea ufahamu wa kutosha mosi kuhusu Biblia inasema nini juu ya ulimi na pili namna ya kukitumia kinywa chako vizuri ili kuamua hatma nzuri ya maisha yako.
‘Na ulimi wangu utanena haki yako, Na sifa zako mchana kutwa’ (Zaburi 35:28)
Utukufu na Heshima vina wewe Yesu wangu, wastahili BWANA.
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, iwe nanyi.

WAKATI NA MAJIRA

ISHI KATIKA WAKATI NA MAJIRA

Mungu alipo muumba mwanadmu alikuwa na mpango mzuri haijarishi kabila lako, kimo chako, utajiri wako, bara lako au nchi uliyozaliwa. Lakini pamoja na hayo mwanadamu huyu huyu akamkosea Mungu kupitia udanganyifu wa Ibilisi Shetani na kuondokewa na utukufu.
Hivyo Mungu akaandaa mpango wa kurudisha uhusiano uliokuwa umepotea kupitia jina la mwanaye wa peke Yesu Kristo ili kila amwaminiye sipotee bali awe na uzima wa milele. 
Yohana 3:16

Si kwamba tulistahili kufanyiwa hivyo ni neema tu ya Mungu baada ya kuona adha na mateso tunayopata, kwa maana nyingine ni kwamba tusingeweza kulipa gharama lakini Mungu kwa kuwa ni mwingi wa rehema akamua kumtoa mwanaye ili tuhuishwe kwa damu yake, kwahiyo tumeokolewa kwa neema, kwanini nasema kwa neema kwasababu Neema ni stahili ambayo mtu hupata/kupewa hata kama mtu huyo hakustahili.
Waefeso 2:1-5


Sasa watu wengi wamekuwa wakilaumu wanapopitia changamoto, Sulemani ameeleza kuwa kila jambo kuna majira yake na wakati wakila kusudi chini ya mbingu na ameeleza nyakati nyingi sana.
Mhubiri 3:1-12

 Lakini baadaye alipozieleza nyakati hizo na majira tena akasema "Siku ya kufanikiwa ufurahi, na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya ...
Mhubiri 7:14.
Mungu ndiye anayejua changamoto, majaribu na wakati mgumu unaopitia, hivyo mtumaini yeye ili ufike mwisho wako salama na kesho yako iko mikononi mwake, Ayubu aliona amelemewa akatambua kwamba hakuja na kitu duniani atarudi bila kitu akasema " Lakini yeye aijua njia niendeayo akisha kunijaribu nitatoka kama dhahabu. "
Ayubu 23:10
 Mungu akubariki jipe moyo mkuu kwa hilo linalokusumbua utashinda

Friday, July 20, 2018

WITO WA UONGOZI


Wito Wa Mungu Kwetu Wa Kuongoza


“Natufanye mtu kwa mfano wetu….. akatawale”. (Mwanzo 1:26)


Kwa karne nyingi wakristo wamejadiliana juu ya suala la uongozi. Je, kuongoza ni kibiblia? Je, sisi hatukuitwa ili kuwa wafuasi badala ya viongozi? Je, hatukuitwa kuwa watumishi badala ya watawala? Je, tunaweza kuwa wakweli na kuamini kuwa uongozi ni wazo la kibiblia?


Tunapojifunza Biblia kwa karibu zaidi tunaona kuwa uongozi ni wazo la Mungu hasa. Si kwamba tu Mungu ni kiongozi wa juu kabisa lakini ametuita sisi pia kuongoza.


Tumezaliwa Kuongoza


            Fikiria hili. Maelezo ya mwanzo ya mwanadamu katika Biblia yanahusisha uongozi. Mungu alituumba kuongoza, kuwa na mamlaka na kutawala. Kulingana na Mwanzo 1:26 – 31, mimi na wewe tulizaliwa ili kuongoza. Soma kwa undani maandiko haya …


“Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi”. (Mwanzo 1:26)


1. Kuumbwa kwa mfano wa Mungu kunamaanisha tuliumbwa ili ________.


Kulingana na mstari wa 26, tuliumbwa kwa mfano wa Mungu. Hii inamaana gani? Kidokezo kimoja kinapatikana katika kifungu kinachofuata “na wakatawale” Sehemu ya maana ya kuwa mfano wa Mungu ni kujua tuliumbwa kuongoza na kutawala.


2. Mungu aliwapa wanadamu _________ juu ya dunia yote


            Tunapaswa kujisikia vizuri juu ya nafasi mbili tulizo nazo. Nafasi ya kwanza ni kuwa chini ya mamlaka ya Mungu. Nafasi ya pili ni kuwa na mamlaka juu ya ulimwengu. Mungu ametupa sisi wito huu. Ni lazima tugundue ina maana gani kuongoza kama Mungu afanyavyo.
         3. Kama Mungu ametuambia tutawale, tunao________ wa kufanya hivyo.


            Mungu kamwe hatuamuru kufanya kitu bila kutupa uwezo wa kufanya kitu hicho. Wewe na mimi tuna uwezo wa kuongoza kwa sababu Mungu alituumba na kutuamuru kufanya hivyo. Kwa kuzingatia vipawa vyako na haiba yako una uwezo wa kuongoza katika maeneo fulani.


            Kuwa Chumvi Na Nuru

            Katika agano jipya, Mungu anathibitisha wito huu wa kuwashawishi wengine. Angalia Mathayo 5:13-16:  “Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima, wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hiyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni”.


Chumvi huathiri chakula tunachokula. Nuru huathiri nyumba tunazoishi. Yesu anatuita kukumbatia wito wetu wa kushawishi na kuangaza popote tuendako. Mtume Paulo alitilia maanani wito huu pale aliposema:


“Basi tukiijua hofu ya Bwana, twawavuta wanadamu…” (2 Wakorintho 5:11)


Ruhusa ya kimungu ya kuongoza


Wengi wetu hujisikia kama Musa alivyojisikia alipokabiliana na Mungu katika kichaka kilichowaka moto katika Kutoka 3 – 4. Alijisikia mpungufu na asiye na maandalizi ya kuongoza. Lakini hicho ndicho Mungu alichomuitia kufanya. Viongozi wengi wakuu wa Biblia waliogopa na kuukimbia wito huo. Ilibidi Mungu awape ruhusa ya kufanya hivyo.


Wengi wetu tunaweza kutoa sababu zinazotufanya kutokuongoza vizuri, kama Musa alivyofanya. Mungu alipomuita, mara moja, alikuwa na sababu tano za kushindwa kuongoza. Tambua jinsi Mungu alivyojibu kuhusu sababu hizo.


Udhuru wa kwanza: Mimi ni nani? (Kutoka 3:11)

Musa alisumbuka juu ya utambulisho wake. Hakujisikia kama alikuwa anastahili. Alifikiri Mungu alichagua kiongozi asiye sahihi. Mwitikio wa Mungu si kitu wewe u nani. Nimekuita. Niko pamoja na wewe.


Udhuru wa pili: Wewe ni nani? (Kutoka 3:13)

Musa alisumbuka na uhusiano wa karibu. Hakumjua Mungu kiasi cha kutosha kumuelezea kwa watu. Uhusiano wake na Mungu ulikuwa dhaifu. Mwitikio wa Mungu: Mimi Niko ambaye Niko. Mimi ni kila kitu unachohitaji.


Udhuru wa tatu: Itakuwaje wasipokubali kusikiliza (Kutoka 4:1)

Musa alisumbuka na woga. Aliogopa juu ya mwitikio wa watu juu yake. Mwitikio wa Mungu katika utimilifu wangu, watasikiliza. Nitumaini mimi.


Udhuru wa nne: Sijawahi kuwa mnenaji mzuri (Kutoka 4:10)

Musa alisumbuka na upungufu. Nani angemfuata wakati hakuweza kuzungumza vizuri? Mwitikio wa Mungu: Fikiri nani aliufanya mdomo wako? Mimi ndiye chanzo cha vipawa vyako.


Udhuru wa tano: Najua unaweza kupata mwingine (Kutoka 4:13)

Musa alisumbuka na kujidharau. Alijilinganisha na watu wengine wenye uwezo zaidi yake na akajiona hafai. Mwitikio wa Mungu. Sawa, utakwenda na Haruni… lakini bado nakuita wewe.


SWALI: Una udhuru gani kwa kutokuongoza vizuri? Unaamini mwitikio wa Mungu waweza kuwaje?





IJUE NAFASI AMBAYO MUNGU AMEKUPA





MAENDELEO

           JINSI YA KUANZISHA BIASHARA Uchumi wa Tanzania umekuwa ukizalisha ajira chache kila siku. Hii imekuwa ikifanya vijana wengi wa...